Men The Podcast - podcast cover

Men The Podcast

Michael Barutiwww.menthepodcast.com
One of the major barriers to men addressing and tackling the challenges they face is the fact that discussion of mental health is largely taboo for Tanzanian men. They’re not expected to open up and talk about their struggles with life. Every two weeks (Fortnightly), on Wednesdays Michael Baruti and Nadia Ahmed present an episode that will discuss the challenges that men go through and offer detailed insight on mental health for men. If you’re interested in Mental Health and are interested in unpacking and unlearning mental health for men in Tanzania, this podcast is exactly what you need
Last refreshed:
Follow this podcast in the Metacast mobile app to refresh it and see new episodes.
Download Metacast podcast app
Podcasts are better in Metacast mobile app
Don't just listen to podcasts. Learn from them with transcripts, summaries, and chapters for every episode. Skim, search, and bookmark insights. Learn more

Episodes

Ep 42 - Unmatched Mindset

Umeshawahi kutaka kufanya kitu ambacho wewe mwenyewe kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwako unafahamu kwamba ni ndoto yako na unatamani sana kuitimiza ila watu wanaokuzunguka wasilione hilo wala kukubaliana nalo? Ulifanya nini? Uliweza kukomaa na kutimiza ndoto zako au uliamua kuua ndoto zako na kuishia kufanya kile ambacho kila mtu alikwambie ufanye? Inahitaji ushujaa, uvumilivu na commitment ya hali ya juu ili kuweza kutimiza ndoto zako, na inakua ngumu zaidi pale ambapo jamii, familia na watu w...

Sep 09, 20211 hr 20 minEp. 42

Ep 34 - To New Hobbies and Trying New Things

Hii ni kwa ajili ya kujaribu kufanya vitu vipya, kwa ajili ya kuwa tofauti na zaidi ya yote, ni kwa ajili ya mabadiliko ya afya ya akili ya Mwanaume wa kitanzania Binadamu wengi sana hua tunaridhika na yale tunayoyajua na yale ambayo tumeyazoea. Na mara nyingi huwa tuna hofu kubwa sana ya kujaribu mambo maya aida kwa sababu ya mazoea au kwa kuhofia matokeo ya lile jambo. Lakini, tutawezaje kuwa watu bora na tutawezaje kubadilika kama hatutaki kujaribu mambo mapya? Danny pamoja na Patrick wameamu...

Sep 04, 20211 hr 11 minEp. 34

Ep 41 - Finding your purpose

Kwa nini unaishi? Ni kipi ambacho unakitaka maishani? Ni kipi unachokithamini? Upo tayari kukifanyia kazi ili kukipata? Upo tayari kuachana na yale ambayo yanasimama katikati ya wewe na kufikia pale unapotaka kufika? Upo tayari kulipa gharama za kuweza kufika pale? Na zaidi ya yote, KWA NINI hicho kitu ni muhimu kwako? Safari ya miasha inakuja na mambo mengi sana, méngine tunaweza yaelezea mengine hatuwezi ila ukweli ni kwamba watu wengi sana bado tupo kwenye safari ya kujitafuta na ya kuweza ku...

Aug 26, 20211 hr 26 minEp. 41

Ep 40 - My Time in Prison

Kutana na Tito Magoti, mwanasheria kijana kutoka Tanzania. Mwaka 2019, alijikuta gerezani ambapo alikaa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Sasa Tito ametoka, anaendelea na maisha yake. Unahitaji nini ili uweze ku “survive” maisha ya gerezani? Watu wako wanaokuzunguka inabidi wafanye nini ili waweze endelea kukutia moyo? Nini kilichompa Tito nguvu na moyo wa kuishi gerezani na kumfanya asikate tamaa ya maisha? Baada ya kutoka gerezani, jamii imempokeaje Tito? Yupo tayari kuishi maisha ya mtu anayeangaliwa...

Aug 12, 20211 hr 8 minEp. 40

Ep 39 - Men do communicate, differently

Wanaume hawajui namna ya bora ya kuwasiliana, kuanzisha mazungumzo ya muhimu na inawezekana hawajui kabisa kuongelea wanayoyapitia, wanayoyafikiria au kuelezea hisia zao wakiwa kwenye mahusiano, hii ni dhana iliyojengeka kwa watu wengi sana, je ina ukweli wowote? Baadhi ya wanaume wanapingana na hili, na wanasema si kweli. Wanaume wanaweza sana kuwasiliana, sema tu wanawasiliana kwa namna ambayo ni tofauti na inahitaji muda kuielewa. Michael na Nadia wanazungumza kwa kirefu sana na Gillsant pamo...

Jul 29, 20211 hr 45 minEp. 39

Ep 38 - Ukweli kuhusu nguvu za kiume

Tatizo la nguvu za kiume ni tatizo gani? Linaathiri wanaume wangapi duniani? Chanzo cha hili tatizo ni nini? Matumizi ya dawa za asili kama “Vumbi la Congo” na “Al Kasusi” ni kweli yanasaidia kutatua tatizo hili? Ni tatizo linalotibika? Kuna madaktari wanaoweza kusaidia kwenye hili tatizo? Linahusiana vipi na afya ya akili? Mbona mara nyingine hili tatizo kama linapotea na mara nyingine kama linarudi? Kuna suluhisho la kudumu? Haya ni baadhi ya maswali ambayo wanaume wengi sana hujiuliza kuhusia...

Jul 15, 20211 hr 11 minEp. 38

Ep 37 - Seemingly perfect? Think again (Part 2)

If you were asked the following questions; do you think you have mastered the art/science of life and communication? What does conflict resolution in your relationship(s) look like? Do you think it is possible to love the things that you’ve grown to hate? And lastly but most importantly, what's the importance of self-acceptance and self-awareness in our life journey? - Would you know the answers at the tip of your finger? Welcome, we are thrilled to have you back with us in this second part of o...

Jul 02, 202156 minEp. 37

Ep 36 - Seemingly perfect? Think again (Part 1)

Look, Princely anaendesha kampuni nzuri inayofanya vizuri kibiashara, kampuni yake ilishinda shindano na wakapata hela nzuri tu ya kumwezesha yeye kuendelea kutimiza ndoto zake. Anaishi kwenye eneo zuri, na ni mtu poa sana. Hawezi kuwa na tatizo, na afya yake ya akili haiwezi kuwa challenged, right? WRONG Ukweli ni kwamba, si mara zote tuonekanavyo nje ndiyo tulivyo kwa ndani. Unaweza onekana kwamba una kila kitu nie, ila bado afya ya akili isiwe katika mahali sahihi. Inakuathiri vipi? Unatambua...

Jun 17, 20211 hr 1 minEp. 36

Ep 35 - Three Months Paternity Leave

Miezi mitatu ya likizo ya uzazi kwa mwanaume. Inaonekana kama kitu cha ajabu sana hata kukizungumzia, uongo au kweli? Can you imagine a man, a Tanzanian man to be precise taking three months paternity leave? Well, kama hauamini basi fahamu kuwa yupo mtu aliyefanya hivyo, na muda huu ulibadilisha kabisa maisha yake na mtazamo wake kwa ujumla juu ya uzazi na malezi kwa ujumla. Lakini pia tunazungumzia kwanini wanaume walio wengi hupata changamoto kubwa pale wanapopata watoto wachanga na namna gani...

Jun 03, 20211 hr 20 minEp. 35

Ep 33 - Blended Family, Fatherhood & Therapy

Moja kati ya mambo ambayo yapo kwenye jamii zetu ila hayazungumziwi sana ni namna ya kuweza kuwa baba bora na mume bora pale ambapo unaishi katika familia iliyochanganyika (Blended Family). Lakini ni namna gani unaweza kufikia hilo lengo pale ambapo kuna zaidi ya baba mmoja kwenye familia, zaidi ya mama mmoja, zaidi ya bibi na babu mmoja kwa kila upande na zaidi ya mtoto mmoja ambar yupo katikati ya haya yote? Michael na Nadia wameingia ndani na kulijadili hili kwa kina na ndugu Reuben Ndege ana...

Apr 30, 20211 hr 22 minEp. 33

Ep 32 - Unpacking The Man Box

“The man box” Hili ni box ambalo sio rasmi, na limetengenezwa na Jamii linalotumika kuchanganua tabia za mwanaume. Kwenye box hili kuna mazuri kuhusu wanaume, lakini pia kuna vitu ambavyo sio sahihi kuendelea kuvishikilia kwa mwanaume anaetaka kubadilika na anaetaka kuwa bora. Lakini, nani alianzisha “box” hili? Mambo gani mazuri yanayopatikana katika hili box? Yepi ambayo si mazuri na hayafai? Na pia, namna gani wanaume tunaweza kuanza kuchambua na kutoa yasiyofaa kutoka kwenye hili box? Ungana...

Apr 16, 202158 minEp. 32

Ep 31 - How Do You Move On From A Big Loss?

KIla kitu kilikua kinaenda vizuri sana kwa Gabriel, wakati akiwa anasoma chuo kikuu alibahatika kupata mwenza wa maisha. Wakajaliwa mtoto mzuri wa kiume, na baada tu ya kumaliza chuo wote wawili wakaamua kufunga pingu za maisha. Familia nzuri, na changa hii ni ndoto ya watu wengi, si ndiyo? Lakini, wakati wa taratibu za kujifungua mtoto wa pili, mke wa Gabriel anafariki, na mtoto anapona. Katika umri mdogo wa miaka 30, Gabriel anapoteza mwenzi wake wa maisha, na anaachiwa watoto wawili ambao ina...

Apr 02, 20211 hr 13 minEp. 31

Ep 30 - Lessons From My Father

Vuta picha, wewe ni kijana mdogo wa kiume, una miaka 7, unaishi na baba na mama na wadogo zako. Baba ni mwanasheria anayechipukia kwa kasi sana katika Serikali ya nchi changa ya Tanzania, mnaishi kwenye nyumba zuri ya hadhi ya juu na kila kitu kipo sawa. Then linatokea janga kubwa sana katika familia, unapoteza wadogo zako wote, mama anapelekwa jela na wewe unalala hospitali kwa miezi kadhaa ukiwa haujitambui. Pindi tu unapopata fahamu, baba anakuchukua unaenda kuishi nae nje ya nchi mkiwa mpo w...

Mar 12, 20211 hr 21 minEp. 30

Ep 29 - Why men cheat?

We are back with a million dollar question, Why do men cheat? Kwa walio wengi hili ni swali ambalo bado halijapatiwa jibu. Kwanini wanaume wanakosa uaminifu kwenye mahusiano? Je ni tabia? Ni mapokeo? Ni swala ambalo jamii halijaliongelea kwa undani? Je lina suluhisho? Michael Baruti pamoja na Nadia, wanazungumza na John (sio jina lake halisi) na kujaribu kuliangalia kwa kirefu hili swala.

Feb 19, 20211 hr 13 minEp. 29

Ep 28 - Fatherhood & Parenting

Moja kati ya vipimo vya mwanaume bora kwa watu walio wengi ni namna mwanaume huyo anavyobeba majukumu yake kama baba. Lakini baba ni nani? Kazi ya baba ni nini? Baba anatakiwa awe vipi? Nini kinamfanya mtu kuwa baba bora? Nimelelewa na baba bora? Mimi ni baba bora? Nataka kuwa baba bora? Nitaweza kuwa baba bora? Nini nifanye ili niweze kua aina ya baba ambae mwanangu anahitaji? Haya ni baadhi ya maswali ambayo wanaume wengi sana hujiuliza pindi linapokuja suala la kuwa mzazi na suala la malezi k...

Dec 18, 20201 hr 15 minEp. 28

Ep 27 - Manhood & Masculinity vs GBV

Meet Mr Anders Sjöberg. Mr Sjöberg is the ambassador of Sweden to the United Republic of Tanzania. Today at the Men. Men. Men. Podcast, on episode #27, we have the honor of sitting down with him at his beautiful residence in Oysterbay, Tanzania and discussing on GBV focusing on Men spaces. His inputs expressed the similarities and differences that both Tanzanian and Sweden Men poses when it comes to dealing with the victimized gender. The solutions that are being implemented, what works and what...

Dec 04, 202041 minEp. 27

Ep - 26 - Kupiga Chabo & Mental Health

Kupiga chabo, kula deo, kupiga kideo, kuchungulia.(Voyeurism). Kama ni mtoto wa kiume ambae umekua hapa hapa nchini Tanzania, basi haya si maneno mageni na wengi sana wamekua wakiona hili ni jambo la kawaida la kufanya kwenye jamiio. Si jambo jema, si jambo la kujivunia LAKINI pia si jambo ambalo watu wanaliongelea. Je unafahamu kua kuna uhusiano wa afya ya akili na tabia hii? Unafahamu kua kuna urahibu (Addiction) ambayo inaweza kutokana na hiki kitendo? Nini chanzo chake? Kinaweza kuathiri vip...

Nov 20, 202055 minEp. 26

Ep - 25 - How Trauma Affected My Speech

Ally Abdallah, alimpoteza baba yake akiwa na umri wa miaka mitano. Baada ya hapo, maisha yake hayakua sawa tena. Ally alipata kigugumizi jambo ambalo lilimpelekea kua na ukuaji tofauti na watoto wengi wa umri wake. Akiwa shule ilimlazimu kuficha kua ana kigugumizi, akiwa nyumbani watu walikua wakimshurutisha kua ajitahidi kuongea vizuri. Unadhani kuishi hivi ni rahisi? Kutana na Ally Abdallah, a comedian ambae anaamini kile anachosema ni muhimu zaidi ya jinsi anavyokisema, Kigugumizi hakijamrudi...

Nov 06, 20201 hr 7 minEp. 25

Ep - 24 - Becoming Your Own Man

Hebu fikiria, mzazi wako anakupeleka shule binfasi, tena ya gharama kweli kweli kwa ajili ya elimu yako ya msingi. Unafanya vizuri, unachaguliwa kwenda shule ya Sekondari halafu ghafla baba anarudi nyumbani na kukwambia “Unajua kusoma na kuandika, inatosha. Silipii gharama yeyote ya wewe kuendelea na shule. Computer hii hapa, internet hii hapa, fanya unachoweza” Hivi ndivyo ilivyokua kwa Mike Mushi, mmoja wa waanzilishi wa mtandao maarufu wa “Jamii Forum”. Msikilize wiki hii kwenye Men, Men, Men...

Oct 23, 20201 hr 12 minSeason 2Ep. 24

Ep - 23 - Male Infertility

Kupata mtoto ni jambo la heri, kupata mtoto ni jambo la baraka. Binadamu walio wengi wanatamani sana kupata baraka hii ya kujaliwa mtoto LAKINI sio kila mtu ana uwezo huu wa kupata mtoto. Wakati mara nyingi maongezo mengi yamekua yakielemea upande wa wanawake ambao hawawezi kupata Watoto, ukweli ni kwamba hata kwa wanaume kuna changamoto zake ila tu hua haziongelewi kiundani na kwa ukubwa wake. Kwenye “Episode” ya leo, Michael na Nadia wanazungumza na Dr France Rwegoshora ambae ni Daktari bingwa...

Oct 09, 202047 min

Ep - 22 - Life in the Public Eye

Una ndoto za kua maarufu nchini Tanzania? Una ndoto za kufahamika na kila mtu kujua jina lako, na sura yako kufahamika kila sehemu? Uko tayari kukabiliana na matokeo ya umaarufu wako? Unadhani Maisha ya watu maarufu ni rahisi na yenye furaha muda wote? Episode hii imezungumza na Dr Hamis Kigwangalla ambae ni Waziri wa Maliasili na utalii nchini Tanzania kuhusu “Life in the Public Eye” au Maisha kwenye macho ya umma.

Sep 25, 20201 hr 20 min

Ep - 21 / Self Care/ The Value of Protecting Your Energy

Hakuna mtu aliyeletwa duniani akiwa anajua kila kitu, hakuna mtu ambae ni mkamilifu wa kila kitu na hakuna mtu ambae hastahili kukua na kubadilika (Evolve and Grow) Lakini kukua na kubadilika kwa mwanaume yeyote au mtu yeyote kunaanza pale anapojitambua na kuanza kujipenda na kujijali zaidi yeye hususani kwenye swala la afya ya akili, mwili na roho. Mara nyingi sana jamii yetu haimpi mwanaume nafasi ya kubadilika na nafasi ya kujifunza kutokana na makosa ya nyuma au nafasi ya kubadilika na kua b...

Sep 11, 20201 hr 7 min

Ep 20 - Ujasiriliamali & Mental Health

ARE YOU MENTALLY STRONG TO BE AN ENTERPRENEUR? Kwa namna moja au nyingine, watu wengi tunawatazama wafanyabiashara na wajasiriamali kama watu ambao wamefanikiwa na wanaishi kwa kupigania ndoto zao. Watu tulio wengi tunatamani kuishi na kufanya kama wanavyofanya wao, na wengine wanafanya ionekana kua ni rahisi kua mjasiriamali na mfanyabiashara nchini Tanzania, si ndio? Well, ukiachana na maisha tunayoyaona kwa juu, unajua gharama za kua mjasiria mali nchini Tanzania kwa upande wa afya ya akili? ...

Aug 28, 20201 hr 38 minEp. 20

Ep 19 - Growing up without my Mother

Mama, nani kama mama? Hakuna kama mama. Kwa wanaume wengi, mama ndio maana halisi ya upendo. Ukiwa mtoto, mama ni mlinzi, mama ni mtetezi, mama ni muuguzi, mama ni mwalimu, mama ni kila kitu. Na ndio maana wataalam wa masuala ya akili na saikolojia wengi hua wanasema kua mara nyingi sana, mtu wa kwanza kupendwa na mtoto wa kiume anakua ni mama. Frank, ameishi kama “mtoto wa mama” kwa miaka 14, na ghafla Mungu akaamua kumchukua mama yake. Frank aliachwa na wadogo zake wawili pamoja na baba ambae ...

Aug 14, 20201 hr

Ep 18 - Suicidal Thoughts

Kweli Maisha si lele mama, kweli Maisha yana changamoto zake nyimgi tu, na nin kweli kua muda mwingine hua tunazidiwa na ugumu wa Maisha mpaka kutamani tuondoke duniani. Umeshahwahi kufikiria kujitoa uhai wako? Nini kilikusukuma kufanya hivyo? Nini ulifanya ili kuondokana na mawazo hayo? Ulipata msaada wowote mahali popote? Vipi jamii inayotuzunguka? Maswali ni mengi kuliko majibu, na inawezekana baadhi ya maswali yasitoe majibu sasa labda tutakuja kupata majibu yake siku za mbele, ila leo hii M...

Jul 31, 202052 minSeason 2Ep. 18

Ep 17 - Unpacking Abuse

Why do men get abusive? Can men be abused too? What do you do when you’re abused? How do you spot an abuser? Can a person be cured from being abusive? A lot of questions on this episode as Michael and Nadia try to unpack abuse with the help of Isaac Lema from the department of Psychiatry and Mental Health in Muhimbili

Jul 17, 20201 hr 20 min

Ep 16 - Growing up without my Father

our first heroes. But what happens when you realize they are only humans? They have their flaws or sometimes they can not be all we want them to be in our lives? In this episode Michael and Nadia have a talk with Ricky Boshe about him growing up without his father and how that has impacted his life as a man right now

Jul 02, 20201 hr 5 min

Ep 15 - Bado Nipo Nipo Sana

When we were young, we couldn’t wait to grow up, but when we did! Oh what a shock! There was so much we needed to do. We needed to get a job! To succeed! To make money! To get married and to have children! Oh such pressure! In this episode we tackle the pressure of adulthood and how men face it and survive it!

Jun 19, 202046 minEp. 15

Ep 14 - Financial Literacy

We spend years in school and in classes perfecting the knowledge that will help us earn a lot of money, yet we spend no time at all learning how to manage money. For most people, finance literacy is a foreign language. Everybody wants to earn good money; everybody wants to save money and everybody wants to spend money wisely. However, this is easier said than done. On Episode 14, Michael and Nadia have a chat with Sam Ndandala about financial literacy and what it means to men...

Jun 05, 202057 min

Ep 13 - Mwanaume na Familia yake vs Corona na Mambo yake

Mwezi March Mwaka 2020, Tanzania ilitangaza kesi ya kwanza ya mtu aliyegundulika na virusi vya Corona. Kwa Mussa (sio jina lake halisi) hakuona kama hili jambo linamhusu. Musa ana mke ambae ni Daktari, ana watoto wawili lakini pia anaishi na mama yake pamoja na baba mkwe wake. Pale wafanyakazi wanaofanya ofisi moja na mke walipogundulika kua na virusi vya Corona, ilimbidi Mussa aiweke familia yake yote katika “karantini”,na hapo ndipo kazi ilipoanza. Kama mwanaume ambae ni kichwa cha familia, kw...

May 22, 20201 hr 3 minSeason 1Ep. 13
For the best experience, listen in Metacast app for iOS or Android