Wimbi la Siasa - podcast cover

Wimbi la Siasa

RFI Kiswahiliwww.rfi.fr

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Last refreshed:
Follow this podcast in the Metacast mobile app to refresh it and see new episodes.
Download Metacast podcast app
Podcasts are better in Metacast mobile app
Don't just listen to podcasts. Learn from them with transcripts, summaries, and chapters for every episode. Skim, search, and bookmark insights. Learn more

Episodes

Je, mkataba kati ya DRC na Rwanda utaleta amani ya kudumu ?

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, walitia saini mkataba wa amani, chini ya uangalizi wa Marekani, Juni Juni 27 2025, jijini Washington DC, unaolenga kurejesha amani ya kudumu Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana kuyaondoa makundi yenye silaha. Mkataba huu umepokelewa vipi nchini DRC ?

Jul 02, 202510 min

Je, usitishwaji wa vita kati ya Israel na Iran utadumu ?

Israel na Iran zimekubali pendekezo la rais wa Marekani Donald Trump, kuacha kushambuliana baada ya vita vya siku 12 vilivyosababisha vifo zaidi ya 600 nchini Iran na zaidi ya 20 nchini Israeli. Israeli ilianza mashambulio hayo, kwa kulenga vituo vya nyuklia vya Iran kwa lengo la kuizuia kutengeneza silaha za maangamizi. Je, usitishwaji huu wa vita utadumu ?

Jun 25, 202510 min

Nini kipo nyuma ya mkataba wa ushirikiano kati ya Kenya na Falme za Kiarabu ?

Serikali ya Kenya mwezi Januari 2025, ilisaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na nchi ya Falme za Kiarabu kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Mswada huo umezua pingamizi kubwa kutoka kwa wanaharakati, watunga será na wapinzani wa serikali na wanataka wabunge kuufanyia marekebisho. Je, kuna siasa gani kwenye mikataba ya Kimataifa inayotiwa saini kati ya serikali ya Kenya na nchi za kigeni ? Edgar Odari Mkurugenzi Mkuu wa, Econews Africa, na Torosterdt Alenga mchambuzi wa siasa za Ki...

Jun 18, 202510 min

Trump azuia raia wa nchi 12 kuzuru Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ameagiza raia wa nchi 12 hasa kutoka Afrika kutozuru nchi hiyo. Agizo hilo lilianza kutekelezwa Juni 9, 2025. Trump anasema amechukua hatua hii kwa sababu za kiusalama. Wakati hayo yakijiri, maandamano yamekuwa yakishuhudiwa katika mji wa Los Angeles, kupinga sera ya Trump ya kuwasaka na kuwafukuza nchini humo, wageni wanaoishi bila vibali. Tunachambua kwa kina.

Jun 11, 202510 min

Sudan yampata Waziri Mkuu, vita vikiendelea kupamba moto

Uongozi wa kijeshi nchini Sudan mwishoni mwa mwezi Mei, ulimteua mwanasiasa na mwanadiplomasia mkongwe Kamil Idris, kuwa Waziri Mkuu mpya wakati huu vita vikiendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF. Tangu kuanza kwa vita Aprili 2023, watu zaidi ya 20,000 wamepoteza maisha, huku wengine Milioni 15 wakikimbia makaazi yao, wakiwemo zaidi ya Milioni nne ambao wamekimbilia katika nchi jirani kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. Nini hatima ya Sudan ?

Jun 04, 202510 min

DR Congo: Kabila aondolewa kinga ya kutoshtakiwa, aripotiwa kufikia Goma

Maseneta nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemwondolea kinga ya kutoshtakiwa rais wa zamani Joseph Kabila , ambaye ripoti zinasema alirejea Goma usiku wa Mei 25.Kiongozi huyo wa zamani, ameishtumu serikali ya rais Felix Tshisekedi na kuuita ya Kidikteta. Hata hivyo, serikali ambayo inamtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kushirikiana na waasi wa M23.

May 28, 202510 min

Wanaharakati kutoka Kenya wafukuzwa nchini Tanzania

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, akiwemo Martha Karua na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga, walifukuzwa nchini Tanzania, Mei 19, walikokuwa wamekwenda kama mashuhuda wa kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Rais Samia Suluhu Hassan ameonya kuwa nchi yake haitaruhusu wanaharakati kutoka nje, kuvunja amani ya nchi yake. Tunachambua kilichotokea nchini Tanzania.

May 21, 202510 min

Uganda: Serikali yawasilisha mswada bungeni, kutaka raia kushtakiwa kwenye Mahakama za kijeshi

Mswada tata, utakaoruhusu raia wa kawaida kushatakiwa kwenye Mahakama za kijeshi, umewasilishwa bungeni nchini Uganda, Mei 13, 2025. Upinzani unasema, lengo la mswada huo ni kuwalenga wanaopinga kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2026. Kwanini serikali ya Uganda inataka raia wa kawaida washtakiwe kwenye Mahakama za kijeshi ?

May 14, 202510 min

Rwanda na DRC zawasilisha mapendekezo kuhusu mkataba wa amani

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimewasilisha mapendekezo ya rasimu ya mkataba wa amani kwa Marekani, kujaribu kutafuta mzozo wa Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zinatarajiwa kutia saini mkataba wa kudumu mwezi Juni, jijini Washington. Harakati hizi, zitazaa matunda ?

May 07, 202510 min

Kenya: Upinzani utamtikisa Ruto uchaguzi wa mwaka 2027 ?

Wanasiasa wakuu wa upinzani nchini Kenya, wakiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, Aprili 29 2025, walikutana jijini Nairobi kuanza mikakati ya kuunda muungano mpya, kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Je, muungano huu ambao pia umemjumuisha aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i, unaweza kumtikisa rais William Ruto wakati wa uchaguzi huo ?

Apr 30, 202510 min

DRC: Kabila aripotiwa kufikia Goma, huku chama chake kikifungiwa

Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila, Aprili 18, aliripotiwa kurejea nchini na kufikia jijini Goma, linalodhibitiwa na waasi wa M 23. Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa rasmi. Serikali jijini Kinshasa, nayo imesitisha shughuli zote za kisiasa za chama chake cha PPRD. Kabila anashtumiwa na serikali kwa kuunga vitendo vya waasi hao.

Apr 23, 202510 min

Tundu Lisssu afunguliwa kesi ya uhaini, CHADEMA matatani

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Tundu Lissu, Aprili 10 alifunguliwa kesi ya uhaini, baada ya kukamatwa akiwa kwenye kampeni ya kisiasa, kushinikiza mageuzi kwenye mchakato wa uchaguzi, uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.

Apr 16, 20259 min

Tanzania: CHADEMA yashinikiza mabadiliko kabla ya Uchaguzi Mkuu

Mwezi Oktoba 2025, wananchi wa Tanzania, watashiriki kwenye uchaguzi Mkuu, kuwachagua madiwani, wabunge na rais. Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kinashinikiza mageuzi kwenye sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo. Je, kitafanikiwa katika harakati zake ?

Apr 09, 202510 min

Mkuu wa majeshi nchini Kenya akemea wanaomtaka rais Ruto aondoke

Mkuu wa Majeshi nchini Kenya, Jenerali Jenerali Charles Kahariri na Mkuu wa idara ya ujasusi Noordin Haji, wameonya dhidi ya kampeni inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na mikutano ya hadhara ya –Ruto Must Go- au Ruto lazima aondoke, inatishia hali ya kisiasa nchini Kenya na ni lazima, ikome. Je, jeshi la Kenya linaingilia siasa ? Tunajadili…

Apr 02, 202510 min

Harakati za kumaliza mzozo wa DRC, nani atafanikisha ?

Wiki hii tunaangazia kinachojiri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Angola kujiondoa kama mpatanishi wa mazugumzo ya mzozo wa Mashariki mwa nchi hiyo, rais Paul Kagame na Tshisekedi wakutana Doha na mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, yazinduliwa jijini Kinshasa. Wachambuzi wetu ni Mali Ali, akiwa Paris na Francois Alwende akiwa jijini Nairobi.

Mar 26, 202510 min

Nani ataisadia Sudan Kusini, isirejee kwenye vita ?

Sudan Kusini inakabiliwa na wasiwasi wa kujipata tena kwenye vita vipya, kufuatia mzozo wa hivi punde kati ya vikosi vya rais Salva Kiir na Makamu wake wa kwanza wa Riek Machar, baada ya kushambuliana kwenye jimbo la Upper Nile. Nini kinaweza kufanyika kuzuia mzozo mpya ? Wachambuzi wetu ni Dokta Brian Wanyama, kutoka Kenya na Hamdum Marcel akiwa Mwanza, Tanzania.

Mar 19, 202510 min

Serikali ya umoja wa kitaifa itasuluhisha mzozo wa DRC ?

Wakati huu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inapoendelea kukabiliwa na changamoto ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya waasi wa M23 kuingia katika miji ya Bukavu na Goma, rais Felix Tshisekedi ametangaza mpango wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwashirikisha wanasiasa wa upinzani. Tunajadili iwapo hatua hii itasaidia kutatua mzozo wa mashariki mwa DRC.

Mar 12, 202510 min

Je, Raila ataegemea upande gani wa kisiasa ?

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga , yupo kwenye harakati za mashauriano ya kisiasa na wafuasi wake, kabla ya kutangaza mustakabali wake wa kisiasa baada ya kukosa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Je, Raila ataegemea upande gani ? Tunachambua.

Mar 05, 202510 min

Mahamoud Ali Youssouf ashinda Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika

Waziri wa Mambo ya nje wa Djibouti Mahmoud Ali Youssouf alichaguliwa na wakuu wa mataifa ya Afrika Februari 15 2025, kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika na kumshinda mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga. Tunachambua ushindi wake na kazi kubwa inayomsubiri

Feb 19, 202510 min

Je, maazimio ya jumuiya za EAC na SADC kuhusu DRC yatatekelezwa ?

Makala ya Wimbi la Siasa wiki hii tunaangazia maazimio ya wakuu wa serikali na nchi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC waliokutana Februari jijini Dar es Salaam, kuthathmini hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Miongoni mwa maazimio hayo ni usitishwaji wa vita bila masharti kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa DRC na kutoa wito wa mazungumzo. Wachambuzi wetu ni Chube Ngorombi akiwa Goma, na Francois Alwende akiwa jijini Nairobi.

Feb 12, 202510 min

Nini hatima ya Afrika baada ya Trump kusitisha misaada ?

Rais wa Marekani Donald Trump, baada ya kurejea madarakani Januari 20, ametangaza hatua ya serikali yake, kusitisha misaada hasa ya kifedha kwa nchi za kigeni, kupitia Shirika la Misaada ya Kimataifa (USAID). Hatua hii inamaanisha nini hasa kwa mataifa ya Afrika ? Tunajadili hili kwa akina na Suba Churchil, rais wa kituo cha taifa cha mashirika ya kiraia akiwa jijini Arusha Tanzania.

Feb 05, 202510 min

Nini suluhu ya mzozo wa Mashariki mwa DRC ?

Wiki hii mapigano makali yameshuhudiwa jijini Goma, kati ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M 23 wanaoripotiwa kuungwa mkono na nchi ya Rwanda. Nini suluhu ya mzozo wa Mashariki mwa DRC ?

Jan 29, 202510 min
For the best experience, listen in Metacast app for iOS or Android