Baadhi ya hospitali nchini Kenya zinazalisha chakula kuwalisha wagonjwa
Katika mkakati wa kuboresha lishe,hospitali zinatumia vipande vya ardhi zao kukuza chakula kuwalisha wagonjwa wao
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Katika mkakati wa kuboresha lishe,hospitali zinatumia vipande vya ardhi zao kukuza chakula kuwalisha wagonjwa wao
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema polisi wenye changamoto za afya ya akili hawatafukuzwa kazi bali watapewa matibabu stahiki Kumeshuhudiwa hivi karibuni visa vya polisi kutumia silaha zao visivyo na utendakazi wao kukosolewa na raia pamoja na wanaharakati wa haki
Hivi majuzi bunge la Uingereza limepitisha mswada wa kuhalalisha huduma ya kusaidiwa mtu kufa Huduma hii itatekelezwa katika hospitali chini ya usimamizi wa wahudumu wa afya ,kwa watu wazima wanaougua magonjwa yasiyopona . Watalaam wa afya wanasisitiza kuwa hatua hiyo sharti mgonjwa kuridhia bila kushinikizwa .
Takwimu zinaonesha watu wengi kupatwa na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kuishi bila kufanya mazoezi na kula vibaya Sera hii itatoa mwongozo wa taasisi za serikali na binafsi kuweka mikakati ya kuruhusu mazoezi ya kila mara wakati wa kazi au nje ya kazi
Kila siku mwili wako hukuzungumzia na ni jukumu lako kusoma mwili wako na kuelewa unasema nini au unakuonya kuhusu nini Baadhi ya matatizo ambayo unaweza kujiepusha nayo ni matatizo ya afya ya akili ,kufeli viungo muhimu au mifumo yako ya afya. Na ili kuhakikisha mwili wako unazungumza na kutoa taarifa iliyo sahihi kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kwa mfano kupata muda wa kutosha kulala,kupata lishe bora na kufanya mazoezi
Matatizo ya tezi koo yanaweza kujidhirisha kwa dalili kama vile msongo wa mawazo,kukosa usingizi,kiwewe na mtu kukosa ari ya chochote maishani Katika makala haya ,tunamtambulisha Daktari Violet Oketch anayesimamia kitengo cha afya ya akili katika hospitali kuu ya rufaa nchini Kenya ya Kenyatta. Daktari Violet anafafanua ufungumano kati ya matatizo ya tezi koo na matatizo ya afya ya akili. Aidha afisa mkuu mtendaji wa kikundi cha kuhamasisha kuhusu matatizo ya tezi koo,Thyroid Disease Awareness K...
Misri ipo kwenye njia panda kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara. Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tu...
Kabla mgonjwa yeyote kuanzishwa kwenye matibabu, awe ana tatizo la tezi koo kuzalisha homoni kupitiliza au kushindwa kuzalisha, ni sharti vipimo maalum kufanyika Kipimo cha kwanzo ni inaangazia homoni tofauti inayozalishwa na tezi koo na hii mtu yeyote anaweza kufanya katika wakati wa kufanya vipimo kujua hali yake ya afya ,hapa mtu si lazima awe ameonesha dalili za tezi koo kuwa na tatizo. Kipimo cha pili ambacho ni muhimu huzingatia zaidi viwango vya homoni tatu muhimu zinazozalishwa na tezi k...
Matatizo ya tezi ya koo ,kwa kawaida yananaletwa na upungufu au wingi wa madini aina ya iodine ambayo huzalishwa na tezi (thyroid gland). Homoni inapokuwa kidogo hali ambayo inafahamika kama Hypothyroidism, hii inaashiria kwamba tezi inafanya juhudi za hali ya juu kutafuta madini hayo . Mtu aliye na hali hii ,anakuwa hana nguvu ,nywele kudondoka na hata mzunguko wake wa mwezi wa damu huvurugika. Madini hayo yanapokuwa mengi inamanisha tezi inafanya kazi kupitliza kuzalisha homoni iliyozidi kweny...
Misri imepambana kwa karibu miaka 100 kabla kupata cheti cha WHO cha kufaulu kutokomeza Malaria Oktoba 2024 Katika mkakati ambao umetumia Misri kuangamiza Malaria ni udhibiti wa Mbu,ambapo serikali iliwekeza kwenye kupiga dawa kwenye maeneo yanayoweza kuwa makazi ya mbu . Ufuatiliaji na ubainishaji wa haraka umechangia pia pakubwa kuushinda ugonjwa wa Malaria ,mkakati ambao pia jamii ilibidi kushirikishwa. Kitengo cha afya ya umma kimekuwa kikifanya hamasisho kwa wanajamii kukumbatia mbinu za ku...
Ongezeko la magonjwa ya milipuko linaibua swala la kwa nini watalaam wa wanyama hawahusishwi kikamilifu katika mifumo ya afya ya binadaam Mpango wa one Health Approach unaonadiwa kwa sasa kwa mataifa ,unahimiza kuipa kipau mbele afya ya wanyama ,ili kuchangia siha njema ,usalama wa chakula na maendeleo endelevu .
Kumekuwa na malalamishi ya maziwa yaliyo kwenye soko kusababisha madhara ya kiafya Watalaam wa afya ,bodi inayosimamia bidhaa za maziwa nchini Kenya na wanavetirinari wanasema matatizo hayo huenda yanatokana na uzembe wakati wa uchakataji maziwa ,uhifadhi na pia wafanyabiashara wenye pupa.
Baadhi ya changamoto zinazokumba sekta ya tiba asilia ni mwitiko na ukosefu wa sheria za kuisimamia katika nchi mbali mbali
Waganga wa tiba asilia wana mchango katika ulimwengu wa uzalishaji dawa
Kuna idadi kubwa ya watu wanaoshindwa kupata maji salama kwa matumizi ya nyumbani ,hospitali na hata mashamba Uhaba wa maji unaorodheshwa kuwa sababu kubwa ya watu kukosa chakula, kujikimu katika nchi zinazoshuhudia migogoro. Katika nchi kama Sudan na DRC kuna ripoti za hospitali ,kambi za wakimbizi kukosa moja hivyo mashirika ya kimsaada yanapata changamoto kuwahudumia wakimbizi
Ukosefu wa lishe bora huathiri afya na elimu nchini Kenya Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la linalowahudumia Watoto (UNICEF) imeonesha kuwa takriban watoto milioni mbili nchini Kenya wanakabiliwa na matatizo yanayotokana na utapiamlo. Mipango ya lishe bora shuleni eneo la Nyanza na maghari mwa Kenya umeonekana kuwa suluhu huku wanafunzi wakipata vyakula vilivyo na virutubishi bora vinavyosaidia kuboresha kinga ya mwili,hivyo kuimarisha afya .
WHO imetaja ukosefu wa huduma za kuokoa maisha wakati wa kujifungua huchangia vifo vingi vya wanawake waja wazito Huduma hizo za wanawake hata hivyo zina bei kubwa
Serikali za Afrika zitalazimika kuchangia ufadhili wa mipango ya kupambana na Malaria kufidia pengo kubwa la ufadhili Muungano wa viongozi wa Afrika wa kupambana na Malaria ,Africa Leaders Malaria Alliance unasema Afrika inahitaji dola bilioni 5 nukta nane mwaka huu wa kifedha hadi 2026. Hali hii pia imechangiwa na Marekani kukata ufadhili wa misaada kwa nchi za kigeni
Mamia ya wakaazi wa kaskazini mashariki mwa Kenya maeneo yanayopakana na Somalia na waathiriwa wakubwa wa mzozo wa Somalia hawajakuwa na maji masafi , hali hiyo ikizidisha mgogoro wa kijamii ndani ya jamii hii ya wafugaji wanaotokea upande wa Kenya na upande mwingine wa Somalia. Kukabili hali hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu , International Committee of the Red cross ,ICRC , shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya ,Kenya Red Cross,KRC katika mkakati wa kuleta amani na ustawi imekuwa...
Katika siku za hivi punde magonjwa ya milipuko imeripotiwa katika mataifa ya Afrika ,ikiwemo Ebola Marburg na Mpox
Guinea itakuwa ni taifa la nane la Afrika kuthibitishwa kuangamiza ugonjwa wa malale Guinea imekuwa ilishiriki katika majaribio ya matibabu ya ugonjwa wa malale ambayo yalifanyiwa utafiti mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Timu ya madaktari kutoka DRC na Guinea walishirikishwa kwenye majaribio hayo na kwenye makala haya tumezungumza na Dkt Chirac Bulanga kutoka DRC
DRC imeripoti maambukizi ya Ukoma mwisho wa mwaka jana na pia mwaka huu Ukoma ni ugonjwa unaoathiri sana ngozi na unaweza kuharibu baadhi ya viungo kama vile mikono ,miguu na hufanya mtu kutengwa na jamii
Kumeendelea kushuhudiwa kwa idadi kubwa ya watu wanaougua mafua au magonjwa yanayoathiri mfumu wa kupumua mwezi Januari ambao una joto jingi na vumbi. Hii inajiri wakati China ikiwa imeripoti mlipuko wa ugonjwa wa Human metapneumovirus ,HPMV unaofanana na COVID 19 . Daktari Juma Maleve kutoka Hospitali ya rufaa ya Mombasa ,Pwani ya Kenya anafafanua.
Kwa kitaalam mtindio wa ubongo unaitwa Cerebral Palsy kwa kifupi CP..ugonjwa huu unatokana na jereha kwenye ubongo ambao huwa linafanya mtoto kushindwa kudhibiti misuli ya mwili wake hali inayoweza kusababisha viungo vya mtoto kulegea au kukamaa muda wote. Mtoto anaweza kupata majeraha kwenye ubongo akiwa bado yuko tumboni, wakati wa kuzaliwa au baadae maishani. CP husababisha ulemavu wa kudumu katika maisha yote ya mtoto.