Ni Salama - podcast cover

Ni Salama

Adrian Nzambani-salama.simplecast.com
Ni salama rohoni mwangu ni Podcast inayokusaidia kuboresha mahusiano yako na Mungu kupitia mafundisho mbalimbali yanayotolewa na wahubiri, walimu na wachungaji kiganjani mwako. Tunakusaidia kuweza kuanza siku vyema ukiwa na neno la mungu kama taa itakayokuwa ikikuongoza katika shughuli zako za kila siku. Kupitia Ni Salama tutakuletea mafunzo na masomo yatakayokuwezesha kuelewa zaidi neno la Mungu linalopatikana kwenye Biblia huku tukikuongezea hamu na mvuto wa kuisoma Biblia yako. Karibu
Last refreshed:
Follow this podcast in the Metacast mobile app to refresh it and see new episodes.
Download Metacast podcast app
Podcasts are better in Metacast mobile app
Don't just listen to podcasts. Learn from them with transcripts, summaries, and chapters for every episode. Skim, search, and bookmark insights. Learn more

Episodes

Namna ya kujiandaa kukikabili kipindi hiki cha siku za mwisho (Sehemu ya pili)

Katika siku hizi za mwisho ambazo Yesu anakaribia kurudi dunia lazima ijue, mkubwa kwa mdogo lazima wajue kwamba kurudi kwa Bwana kumekaribia. Biblia inasema na watakatifu na wazidi kujitakasa, wanaofanya kazi ya Mungu na wafanye upesi maana Roho pamoja na malaika na watumishi wanasema njoo, maana yake kuna kitu kinachomzuia asije. Biblia inasema injili ya Ufalme wa Mungu itakapohubiwa kote, anasubiri tufanye kazi yake. Kama umesoma kitabu cha Luka wakati Yesu amefufuka Luka 24:44 Kisha akawaamb...

Aug 14, 201910 minSeason 1Ep. 19

Namna ya kujiandaa kukikabili kipindi hiki cha siku za mwisho

Na Biblia inasema Yesu siku za mwisho hatakuja hapa duniani, kwa sababu maandiko yanasema kile kiti cha enzi kikubwa cheupe, kiti cha hukumu dunia itakimbia na mbingu zitakimbia na kwa sababu hiyo hicho kiti hakitakuwa duniani kwa sababu dunia itakimbia na mbingu zitakimbia. Biblia inasema nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo wamesimama katika kiti cha enzi halafu atasimama pale kama hakimu. Sasa hivi ni mwokozi wako lakini ukikutana naye ng’ambo ya pili kama hujaokoka utakutana naye kama hakimu na...

Aug 13, 201910 minSeason 1Ep. 18

Kama huna uhakika Yesu akikuita muda huu huna uhakika hakikisha leo unaokoka

Kama huna uhakika Yesu akikuita muda huu huna uhakika hakikisha leo unaokoka Wakati fulani tulisafiri na mzungu mmoja alikuwa ni mjerumani toka Arusha kwenda Dar es salaam. Aliombewa lift na mwenzake ili tusafiri naye, tukamuuliza je umeokoka akasema hapana. Yeye anamuabudu shetani na anatoka kanisa linalomuabudu shetani. Nikamwambia hamna kanisa la namna hiyo. Nikamuuliza alikuwa anasali kanisa gani akanitajia kanisa la Kikristo alilokuwa anaabudu kabla ya kuacha. Tukamuuliza tena kwa nini ulia...

Aug 12, 20199 min

Kumwamini Mungu kwa kumfuata Yesu Kristo (Sehemu ya Nne)

Tunapozungumza juu ya kumtumikia Mungu watu wengi sana hufikiria watu wachache tu yaani wahubiri, wachungaji, wainjilisti au wanaofanya kazi kanisani. Lakini kwenye Biblia inasema kila kiungo katika mwili wa Kristo kina nafasi yake na kazi yake kwa hiyo ni mtumishi wa Mungu. Inawezekana usihubiri, lakini pale ulipo ni mtumishi wa Mungu maana yake usimame katika kusudi lake ni kueneza Ufalme wake katika kazi ufanyayo. Hakikisha watu wanamjua Mungu maana Biblia inasema kila aliye mwana anao ushuhu...

Jul 24, 201910 minSeason 1Ep. 17

Kumwamini Mungu kwa kumfuata Yesu Kristo (Sehemu ya Pili)

KUMWAMINI MUNGU KWA KUMFUATA/KUPITIA KWA YESU KRISTO. Ukisoma Luka 8:12 “Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.” Pia Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.” Ufahamu ulioko ndani ya akili zisizofaa zilifanya wamkatae Mungu. Kwa hiyo akili itafanya mtu amkubali au amkatae Mungu. 2 Wakorintho 11:3 “Lakini nachelea; kama yu...

Jul 19, 201910 minSeason 1Ep. 15

Kumwamini Mungu kwa kumfuata Yesu Kristo (Sehemu ya Kwanza)

KUMWAMINI MUNGU KWA KUMFUATA/KUPITIA KWA YESU KRISTO. Hapa nilitaka uone katika ule mji Yesu alimpata mtu mmoja tu kwa lugha ya sasa tungesema “kwenye safari ya Yesu kuingia gharama ya kuvuka na boti kwenda kule na kufanya huduma alimpata mtu mmoja tu kwenye ule mji, na tofauti yao ilikuwa kwenye akili. Ingawa kwenye lile eneo wengine hawakuwa vichaa, haina maana kwamba akili zao zilikuwa huru hazijashikwa. Huyu Mgerasi kichaa alipofunguliwa alikuwa huru na ikawa rahisi sana kwa yeye kumfuata na...

Jul 19, 201910 minSeason 1Ep. 14

Kumwamini Mungu kwa kumfuata Yesu Kristo (Sehemu ya Tatu)

Kwa hiyo tangu wakati ule kuna vitu ambavyo alivyokuwa anafanya moja kwa moja vinazaa tena mfano wa kile kitu alichobeba. Sasa unaweza ukaelewa kwa nini katika kipindi hiki cha Agano jipya ni lazima tuzaliwe kwa mara ya pili. Maandiko yanatuambia ndani yake tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu na Biblia inatuambia tutaishi kwa imani Ni imani ya namna gani? Waebrania anasema Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye y...

Jul 19, 201910 minSeason 1Ep. 16

Tufanye maombi na kuombea akili zetu na kutuondoa katika kushikwa na shetani! Omba sasa

Baada ya sala na mafundisho ya Mwalimu Christopher Mwakasege changia huduma ya Mana Ministries iweze kuendelea, kukua na kufikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi. NAMNA YA KUPATA KANDA, CDs & DVDs BONYEZA HAPA 👉🏼 https://goo.gl/xrSwmN NAMBA ZA SADAKA NA MAOMBI 👉🏼 https://goo.gl/7XcFiP MAOMBI YA KUOKOKA NA KITABU CHA HONGERA KWA KUOKOKA. 👉🏼 https://goo.gl/XKoJNB

Jul 18, 201910 minSeason 1Ep. 13

Weka akiba mapema ikusaidie pale utakapo staafu

Maana akili zako zinakuwa zimebanwa kabisa unapata pesa na unazitumia kienyeji kienyeji tu. Ili uweze kuelewa tafuta watu waliostaafu. Wengi sana wana maisha mabaya na ni wachache sana wana maisha mazuri, kwa sababu wengine walikuwa na maisha mazuri sana walipokuwa kazini. Walikuwa na magari na nyumba kumbe ni za shirika au kampuni ambayo anafanyia kazi lakini sio vya kwake. Maana wakati wa zamani wafanyakazi walikuwa wanapewa kila kitu hadi furniture za ndani, ukiwaona utafikiri ni vya kwao kum...

Jul 17, 201910 minSeason 1Ep. 12

Kutumia Ubongo na akili kufanya maamuzi ya chanzo na matumizi ya pesa zako

UBONGO UNATAKIWA UKUSAIDIE KUWA NA MIPANGO YA KUPATA PESA LAKINI AKILI INATAKIWA ZIKUSAIDIE KUAMUA JUU YA CHANZO CHA KUPATA PESA NA KUAMUA MATUMIZI YA PESA HIZO Kazi mojawapo ya akili ni kutusaidia kupambanua mema na mabaya kwa jinsi ya Ki-Mungu ili tuweze kuchagua mema na kuacha mabaya. Biblia inatuambia kuwa akili zao kwa kutumiwa. haijasema kwa kutegemewa bali ni kutumiwa. Biblia imekataza kutegemea akili bali tunatakiwa tumtegemee Mungu. Shetani akitaka kuvuruga maisha yako atakamata akili z...

Jul 16, 201910 minSeason 1Ep. 11

Jifunze kukaa na mkeo kwa akili na si kiroho, jifunze sasa!

Biblia haisemi wanaume tukae na wake zetu kiroho, kwa hiyo usijaribu kukaa na mke wako kiroho, kaa nae kwa akili. Ndani ya akili hizo Mungu atakupa neema ya kumsaidia kumpa heshima anayostahili. Lakini kuona ile nafasi kwa jinsi ya mwili ni chombo kisichokuwa na nguvu lakini katika ulimwengu wa roho wana nguvu kuliko sisi! Kwanini Mungu ameumba jambo jipya mwanamke atamlinda mwanaume wanawake ni walinzi wazuri sana katika ulimwengu wa roho, wana nguvu za kiroho kuliko wanaume lakini inapokuja kw...

Jul 15, 201910 minSeason 1Ep. 10

Ubongo unaona matatizo akili inaona fursa kwenye hayo matatizo

1 Mambo ya Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.” Nataka uone hapa anaposema walikuwa watu wenye akili za kujua nyakati na kitu cha kufanya kwenye nyakati Kwanini? Kwa sababu ukisoma kile kitabu cha Mhubiri; Mhubiri 3:1-2 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati ...

Jul 14, 201910 minSeason 1Ep. 9

Sio swala la kuishi maisha marefu, ni swala la kuishi kwenye mapenzi ya Mungu

Unaweza ukawa unafurahia biashara uliyonayo na kufikiri kwamba umefika lakini Mungu ana kitu kikubwa kuliko unachofikiri. Ila hujajua kwamba huko ndani yako kuna kitu gani kimekaa na kwanini ndani yako unaona ndoto kubwa au unaona hujaridhika mahali ulipo kumbe Mungu anajaribu kukusukuma kukuonyesha kwamba ndani yako amekuwekea kitu kikubwa kuliko unacho fikiri. Hivyo usitosheke na mahali ulipo kisukume na usonge mbele na ukimwendea Mungu atakuonesha mahali unapotakiwa kuwa. Mungu alimpa Yusufu ...

Jul 13, 201910 minSeason 1Ep. 8

Haijalishi unapitia hali gani na upo kwenye kipindi gani, Mungu yuko pamoja nawe

Mtu aliyekuwa anatakiwa kwenye hii nafasi alitakiwa awe ana akili ya miaka 14 kusaidia Misri na nchi za jirani. Alitakiwa awe ana hekima pamoja na Roho wa Mungu ili kuweza kukamilisha jukumu hilo. Yusufu aligundua kuna kitu Farao alitakiwa akitolee nafasi (position) kwa sababu anaweza patikana mtu mwenye akili lakini asiwe na mahali pa kutumia akili zake. Kuna watu wana akili lakini hawana hekima na wengine wana hekima akili hawana. Yusufu alikuwa na hivyo vyote pia alikuwa na Roho wa Mungu ndan...

Jul 12, 201910 minSeason 1Ep. 7

Akili za mwanadamu zingekuwaje kama tusingepitia dhambi, ungekuwa wapi sasa?

Jana tuliangalia kikwazo cha kwanza ni AKILI KUFUNGWA NA SHETANI na tukaangalia kwenye kile kitabu cha Luka 8:26 - 39 tukaangalia kwa undani pamoja na mistari mingine na maelezo kwa undani. Saa nyingine huwa nawaza sana namna akili ya mwanadamu ilivyo na ambavyo inafanya mambo makubwa je kama tusingepita kwenye dhambi ingekuwaje? Kwa sababu vitu vingi vimebuniwa na akili ya mwanadamu ambayo iko kwenye dhambi na ina kiwango cha kufanya kitu ilichokifanya, sasa fikiria kama asingekuwa na dhambi in...

Jul 11, 201910 minSeason 1Ep. 6

Tumia sala hii kuachilia Damu ya Yesu ifungue akili yako

Weka mikono yako juu ya kichwa ili tufanye maombi ambayo Mungu atafuatilia muunganiko wa ubongo wako na akili zako. Kama kuna mapepo katika akili zako yataachia tu kwa jina la Yesu. Omba Mungu aponye akili zako na kuweka huo muunganiko vizuri kwa Damu ya Yesu. Nyunyiza Damu ya Yesu juu yako. Pia kama hujaokoka hakikisha unaokoka, angalia link ya sala ya Toba na kitabu cha Hongera kwa kuokoka. Pia kama una ndugu yako unataka Mungu amponye akili zake andika jina lake tuma kwa namba za maombi tuliz...

Jul 10, 201911 minSeason 1Ep. 5

Uko mahali kwenye maisha yako kila kitu kimesimama, Yesu anakutafuta

Hii unaweza ukasikia mtu akisema “nimemlea huyu mtoto nikifikiri akili anazo kumbe hana”. Ukishasikia lugha ya nmna hiyo ina maana akili hazifanyi kazi inayotakiwa kwa sababu hamna mtu ambaye hana akili ila kuna namna zimebanwa. Sasa angalia yule kijana wa nchi ya Wagerasi kila mtu alikuwa kamkatia tamaa. Sasa Yesu alikuwa hafanyi jambo lolote isipokuwa kamuomba baba akifanya. Kwa hiyo walikuwa anafanya mapenzi yake maana alikuwa akimuona Yesu kayakamilisha. Yesu aliposema tuvuke mpaka ng’ambo i...

Jul 09, 201910 minSeason 1Ep. 4

Unapookoka neno la mungu huanza kushughulikia akili zako

1 Petro 2:1-2 “Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;” Hakusema maziwa ya Roho amesema maziwa ya akili, Neno la Mungu unalopewa unapookoka mahali pa kushughulika napo pa kwanza ni akili zako ili upate kuukulia wokovu, ndio maana akili zikibanwa haijalishi umeokoka miaka mingapi huwezi kukua kiroho, ndio maana huwezi kujivunia miaka uliy...

Jul 08, 201910 minSeason 1Ep. 3

Nafsi na mwili viliumbwa vimilikiwe na roho

NAFSI NA MWILI VILIUMBWA VIMILIKIWE NA ROHO Zaburi 63:1 “Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.” Mwandishi anamwambia Mungu, “Mungu wangu nitakutafuta mapema”, anaposema nitakutafuta ni roho ya Daudi inamweleza Mungu ya kwamba nitakutafuta mapema. Roho hiyo hiyo inasema kwa niaba ya nafsi, inasema nafsi yangu inakuonea kiu, lakini pia inasema kwa niaba ya mwili inasema mwili wangu wakuonea sha...

Jul 07, 201910 minSeason 1Ep. 2

Akili kufungwa na shetani ili usifikie malengo yako

AKILI KUFUNGWA NA SHETANI. Luka 8:26‭-‬39 “Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na ku...

Jul 06, 201910 minSeason 1Ep. 1
For the best experience, listen in Metacast app for iOS or Android