Let's keep it real, we need each other (Part 1) - podcast episode cover

Let's keep it real, we need each other (Part 1)

Jul 28, 202246 minEp. 56
--:--
--:--
Download Metacast podcast app
Listen to this episode in Metacast mobile app
Don't just listen to podcasts. Learn from them with transcripts, summaries, and chapters for every episode. Skim, search, and bookmark insights. Learn more

Episode description

Ni karne ya 21, na mapinduzi mengi sana ya kimaendeleo yametokea duniani na yanaendelea kutokea. Na tunajua kwamba ili tuweze kuendelea kuwa bora kama jamii na kamą wanadamu basi hatuna budi kuyakumbatia mapinduzi yenye tija na yenye kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu.


Moja ya mapinduzi ambayo kama binadamu tumechelewa sana kuanza kuyapambania kwa nguvu zote ni mapinduzi juu ya usawa wa kijinsia. Hili ni jambo jema na lenye msingi wenye kuleta heri kwa jamii nzima. Lakini, ili mapinduzi haya yafanikiwe na yaweze kufikiwa malengo yanayopaswa kufikiwa basi ni lazima jinsia zote mbili ziweze kushiriki kikamilifu katika mchakato huu.


Swali ambalo tunajiuliza leo kwa undani, ni je wanaume wanashiriki kikamilifu katika mapambano na mchakato wa kuleta haki sawa kwa jamii yetu? Kama wanashiriki, nini imekua mchango wao? Na kama hawashiriki, ni kitu gani kinazuia ushiriki wao kikamilifu? Hofu ya wanaume ni nini kwenye hili? Chimbuko la hofu hiyo ni nini? Na ni vipi tunaweza kumshirikisha mwanaume huyu kikamilifu kwenye hii safari? Sababu kiukweli kabisa, wanaume na wanawake wote wanahitajiana kwa ustawi bora wa jamii


Rolland Malaba A.K.A Madenge amejadili swala hili kwa undani na kujaribu kuchanganua baadhi ya mambo akishirikiana na Michael Baruti pamoja na Nadia Ahmed. Karibu usikilize Sehemu ya kwanza ya maongezi haya

For the best experience, listen in Metacast app for iOS or Android