Ep 44 - Cultural Transition, Cultural Shock & Re-Adjusting - podcast episode cover

Ep 44 - Cultural Transition, Cultural Shock & Re-Adjusting

Oct 08, 20211 hr 32 minEp. 44
--:--
--:--
Download Metacast podcast app
Listen to this episode in Metacast mobile app
Don't just listen to podcasts. Learn from them with transcripts, summaries, and chapters for every episode. Skim, search, and bookmark insights. Learn more

Episode description

Kusoma nje ya nchi ya Tanzania kuna mpa mtu faida nyingi sana ukilinganisha na ambae hatapata nafasi hiyo. Vitu kama ubora wa elimu na “exposure” anayoipata si vitu vya kubeza hata kidogo. Kwa wengi ambao hawakupata nafasi hiyo huwa wanawaangalia waliopata hizo nafasi kama watu ambao tayari njia yao ya mafanikio imeshasafishwa na imeshachongwa kabisa, uongo?


Lakini je, umeshawahi kujiuliza juu ya maisha ya ughaibuni? Ni namna gani watu wanamudu kuishi mbali na wawapendao kwa muda mrefu? Ni vipi wanaweza pambana na changamoto kama zinazotokana na kuwa mbali na nyumbani? Ni namna gani matarajio ya watu waliobaki nyumbani kwa watu hawa hugeuka kuwa mwiba mchungu kwa walio wengi? Tunajua kwanini wengine hushindwa kurudi nyumbani? Na hata wakirudi, tunafahamu wanayoyapitia?


Webiro “Wakazi” Wasira anaketi na sisi na kutuambia namna mabadiliko haya yanavyoweza aidha kumjenga mtu au kumbomoa kabisa na yeye amewezaje kufika hapa alipo? Alipitia yepi? Nini ni uzoefu wake? Msikilize hapa

For the best experience, listen in Metacast app for iOS or Android