Mkataba wa kimataifa wa CITES ulianza kutekelezwa mnamo Julai mosi 1975. Toka wakati huo mkataba huu umeendelea kusaidia dunia kuzuia kupotea kwa kasi kwa spishi mbalimbali za wanyamapori na mimea zilizokuwa katika hatari ya kutoweka.
Jul 21, 2025•10 min
Ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kwenda Tanzania maarufu EACOP umefikia asilimia 62, hivi majuzi raia 26 wa Uganda ambao ni waathriwa wa miradi ya mafuta ya Total ya Tilenga na EACOP wamewasilisha keshi mpya dhidi ya kamuni ya TotalEnergies nchini Ufaransa,
Jul 14, 2025•10 min
Waachuuzi wa samaki na dagaa walilazimika kutumia mbinu za jadi kama vile kuni na makaa kukausha aina hii ya samaki wadogo, dagaa, hali iliyowasababishia hasara na kuchangia uharibifu wa mazingira kwa kutupa taka za samaki ndani ya Ziwa Victoria.
Jul 07, 2025•10 min
Hatua ya serikali ya Kenya kuoiga marufuku matumizi ya takriban viuatilifu au dawa za kuua wadudu takriban 77 kutokana na hofu ya usalama wa dawa hizo kwa mazingira na afya ya binadamu. Baadhi ya viuatilifu vimepigwa marufuku katika soko la kimataifa, kuanzia baranai ulaya, Australia, marekani na Canada, laini viipo kwenye masoko ya nchi za ukanda.
Jul 01, 2025•10 min
Watoto wana jukumu muhimu katika uhifadhi wa mazingira na wanyamapori kwa kushiriki kikamilifu katika mipango kama vile kupanda miti, udhibiti wa taka, na kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mazingira na wanyamapori. Kuwashirikisha watoto katika shughuli hizi kunakuza hisia ya uwakili, kuwaunganisha na mazingira wanayoishi, na kukuza mazoea endelevu kwa siku zijazo.
Jun 23, 2025•10 min
Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kutekeleza lengo nambari 14 la Maendeleo Endelevu, ulifanyika kule Nice, Ufaransa, kujadili mbinu mwafaka za kuhifadhi na kutumia kwa njia endelevu bahari na rasilimali zake, washikadau wakiunda uhusiano mpya kati ya wanadamu na mazingira ya baharini. Mkutano wa kilele ulikamilika Ijumaa tarehe 13 Juni, 2025 wakati huu mataifa yakitarajiwa kukutana mwezi ujao kujadili sheria za uchimbaji madini kwenye kina kirefu cha maji baharini....
Jun 19, 2025•10 min
Mataifa yametakiwa kuchukua misimamo mikali kuhusu uvuvi wa kupindukia, uchafuzi wa mazingira na ulinzi wa mifumo ikolojia ya baharini.
Jun 09, 2025•10 min
Uchafuzi wa taka za plastiki umekuwa kero kwa dunia, na kuhatarisha sayari yetu, vyanzo vya maji lakini pia afya ya binadamu na wanyama. Mataifa kukutana mwezi Agosti katika muendelezo wa majadiliano ya kutafuta mkataba wa kisheria wa kimataifa kukabili tatizo hili.
Jun 02, 2025•10 min
Jumatano ya Mei 28 2025, dunia itaadhimisha siku ya njaa ulimwenguni, siku hii ikilenga kutoa hamasa na kuchochea hatua kuchukuliwa ili kumaliza njaa duniani. Kulingana na ripoti ya kimtaifa ya 2025 kuhusu migogoro ya Chakula, zaidi ya watu milioni 295.3 katika nchi 53 wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula.
May 26, 2025•10 min
Jamii za Pwani ya Kenya, zimekumbatia uchakataji wa plastiki kukabili tatizo la uchafuzi utokanao na taka za plastiki ambapo mujibu wa shirika la mazingira la UNEP, kila siku, kiasi sawa cha malori 2,000 ya kuzoa taka yaliyojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito, na maziwa ya ulimwengu.
May 15, 2025•10 min
May 05, 2025•10 min
Ripoti hiyo mpya ya UN Spotlight initiative, imebaini kuwa mabadiliko yatabianchi yameendelea kuzidisha mogogoro ya kijamii na kiuchumi ambayo inachochea kuongezeka kwa viwango vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.
Apr 28, 2025•10 min
Ripoti ya umoja wa mataifa inaonesha dunia ipo nyuma sana katika kudhibiti ongezeko la joto chini ya nyuzi joto 1.5.
Apr 23, 2025•10 min
Baadhi ya wakulima nchini Kenya wameanza kugeukia matumizi ya mbolea asilia inayonyunyiziwa ardhini ili kunusuru mashamba yao.
Apr 14, 2025•10 min
Kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kwa mujibu wa shirika la hali ya hewa duniani WMO, barafu inayopatikana kwenye milima inayeyuka kwa kasi zaidi na ndio sababu ya umoja wamataifa kutenga Machi 21 kama siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu kuyeyuka kwa barafu hii.
Mar 31, 2025•10 min
Wakulima wadogo wanachangia kwa zaidi ya asilimia 70 uzalishaji wa chakula barani Afrika, hii ni kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo barani, Afdb, wakati uo huo, lengo nambari mbili ya maendeleo endelevu ikinuia kumaliza njaa na kuihakikishia dunia usalama wa chakula kufikia mwaka wa 2030
Mar 28, 2025•10 min
Mar 17, 2025•10 min
Binadamu hutegemea rasilimali za wanyamapori na bayoanuwai ili kukidhi mahitaji yao. Tunahitaji chakula, mafuta, makazi, na hata mavazi. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kwamba mifumo ikolojia inaweza kustawi na mimea na wanyama wanaweza kuwepo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Machi 3 mwaka huu, ilikuwa ni fursa ya kutoa uhamasisho wa umuhimu wa wanyama na mimea pori, ili kuongeza ufahamu wa faida zao, na haja ya kuongeza mapambano ya uhalifu dhidi ya wanyamapori na kusababisha athari kubwa...
Mar 11, 2025•10 min
Taka za kieletroniki zinajumuisha vitu vingi ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira na utupaji ovyo ni chanzo kikuu cha madhara, dutu hizi hatari zikiwa na uwezo wa kuchafua udongo, maji, hewa na vyanzo vya chakula. Shirika la E-Waste Initiative Kenya linatoa suluhu ya taka za kieletroniki. Bonyeza hapa kufahamu zaidi.
Mar 04, 2025•10 min
Mkaa wa Briketi hutengenezwa kutoka kwa vumbi la mkaa wa kawaida, taka za kilimo au mabaki ya mbao, na hutumiwa kimsingi kwa mapishi nyumbani, shuleni na hata katika makampuni. Mkaa huu una faida kwa kuwa unapunguza uchafuzi wa mazingira, kupunguza ukataji wa miti lakini pia huwaka kwa muda mrefu na kwa usawa zaidi kuliko mkaa wa kawaida, na kuufanya kuwa chaguo maarufu kwa kupikia.
Feb 20, 2025•10 min
Makala haya yanazungumzia jinsi Wakulima wengi nchini Kenya wanakumbatia mbinu mpya za kudhibiti wadudu waharibifu wa mimea kwa kutumia madawa ya kiasili badala ya kemikali za viwandani. Kutokana na madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kemikali,wakulima hawa sasa wanageukia madawa hayo asilia kuimarisha mazao na mazingira , Mimea kama vile ,pareto,kitunguu saumu,pilipili na hata mtunguja pori yaani sodom apple sasa inatumika kutengeneza madawa hayo.
Feb 10, 2025•10 min
Utunzaji wa bustani ya nyumbani, ni mbinu mpya ya kilimo inayolenga kutimiza malengo matatu kwa wakati mmoja: kuongeza mapato ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha ustahimilivu, halkadhalika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Bustani ya Nyumbani, kwa kawaida huwa karibu na jikoni au pia kwenye roshani. Bustani hii ambayo mara nyingi hutumia mbolea asilia husaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na pia kutunza udongo. Bus...
Feb 03, 2025•10 min
Rais Donald Trump kwa mara nyingine alitangaza Marekani kujiondoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, hatua ambayo imeibua mjadala wa kimataifa. Tangazo hilo lilikuja huku ulimwengu ukishuhudia viwango vya joto vinavyovunja rekodi na majanga yanayozidi kuwa makali yanayohusiana na hali ya hewa. Lakini wadadisi wa mambo na viongozi wengine wa ulimwengu wanatazamaje hatua yake Trump? Bonyeza usikilize zaidi.
Jan 28, 2025•10 min
Sekta ya mitumba inauwezo wa kuchangia mabilioni ya fedha katika mapato ya taifa, pamoja na kutoa maelfu ya ajira katika mataifa ya bara Afrika na ulaya. Kulinga na utafiti wa Oxford Econimics mwaka uliopita; 2024, sekta ya mitumba pekee ina dhamani ya dola bilioni 8 na imetoa ajiri ya idadi ya zaidi laki moja na elfu 60 kwa vijana nchini Msumbiji , Ghana na Kenya . Lakini hata hivyo wanaharakati wa mazingira wanasema baadhi ya nguo hizo za mitumba zinazoletwa Afrika zinachangia katika uchafuzi ...
Jan 23, 2025•15 min