Hoja za Wahariri - podcast cover

Hoja za Wahariri

The Standard Group PLCwww.standardmedia.co.ke
Wahariri wetu wenye tajriba wanatoa hoja na mitazamo mizito kuhusu masuala yanayogonga vichwa vya habari, kila wiki.
Last refreshed:
Follow this podcast in the Metacast mobile app to refresh it and see new episodes.
Download Metacast podcast app
Podcasts are better in Metacast mobile app
Don't just listen to podcasts. Learn from them with transcripts, summaries, and chapters for every episode. Skim, search, and bookmark insights. Learn more

Episodes

Vita vya Urusi na Ukraine; athari kwa dunia

Mwanahabari mstaafu wa kimataifa, Abdu Mtullya anasema vita vya Urusi na Ukraine havistahili na huenda vikaathiri zaidi uchumi duniani, ikiwamo Afrika. Vita hivyo vimesababisha kupanda kwa bei ya mafuta, Urusi ikiendelea kurusha makombora katika ngome za Ukraine, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu mwaka wa 2014.

Feb 25, 20228 min

Mzozo wa Urusi na Ukraine; Mohamed Abdul-Rahman anachambua

Je, unafahamu chimbuko la mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, athari zake na unamaanisha nini kwa Afrika na dunia nzima? Mwanahabari/ Mhariri mstaafu na mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Mohamed Abdul-Rahman anasimulia.

Feb 22, 202215 min

Hoja za Wahariri: Kitendawili cha mili Mto Yala - ndani ya magunia

Dunia inazidi kushangazwa na suala la mili zaidi ya 20 kupatikana ndani ya magunia katika Mto Yala. Mili hiyo ina alama na ishara za mateso. Je, waliouliwa ni akina nani na sababu za kuuliwa ni gani? Aidha, twajadili siasa za OKA vilevile usajili wa wapigakura wapya. Ali Manzu anawashirikisha wanahabari, Shisia Wasilwa na Kennedy Wandera katika kudadavua masuala haya.

Jan 20, 202243 min

Hoja za Wahariri Podcast: Nchi bila umeme; ni njama?

Kupotea kwa umeme nchini Kenya kwa takribani siku tatu kumechochea ghadhabu. Baadhi wanahisi kwamba ni njama ya wafanyakazi fulani wa kampuni za umeme kusababisha hali hiyo maksudi. Kwamba huenda wanalalamikia mageuzi ya usimamizi katika Kenya Power, ama ni kero la wasambazaji wa kawi kulalamikia viwango vipya vya ada za umeme ambavyo ni vya chini, na kuishia wao kupata hasara. Aidha, tunajadili kujiuzulu kwa Mshirikishi wa Utawala, Bonde la Ufa, George Natembeya ili kulenga kiti cha kisiasa. Al...

Jan 14, 202241 min

Hoja za Wahariri Podcast: Ahadi za wanasiasa; watatekeleza?

Wagombea mbalimbali wa urais nchini Kenya wanazidi kutoa ahadi wanazosema watatekeleza endapo watashinda uchaguzi wa 2022. Katika podcast hii, wahariri Geoffrey Mung'ou, Roselyne Obala na mwanahabari mwandamizi, Mike Nyagwoka wanajadili iwapo ahadi zenyewe zinatekelezeka au la kwa kuweka kwenye mizani ahadi za sasa na za awali.

Oct 16, 202112 min

Hoja za Wahariri Podcast: Raila ni chaguo la Uhuru, huku siasa zikichacha Mlima Kenya

Rais Uhuru Kenyatta amewasihi wanasiasa wa One Kenya Alliance kumuunga mkono Raila Odinga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022, huku pendekezo lake likikataliwa vikali na wanasiasa hao. Aidha, wanasiasa mbalimbali wanazidi kujitokeza kwenye eneo la Mlima Kenya wakishindania udhibiti wa siasa za eneo hilo, Uhuru anapoelekea kustaafu. Je, kati ya William Ruto na Raila Odinga, ni nani atakayenufaika katika siasa za Mlima Kenya na ni nani atakayepoteza? Eneo la Mlima Kenya litaamua siasa za 2022? Wawaniaj...

Aug 13, 202127 min

HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Kivumbi kati ya Jubilee na UDA Kiambaa na Muguga

Baada ya chama kipya cha UDA kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye eneo la Kiambaa, kisha Jubilee kukishinda kiti cha uwakilishi wadi Muguga, kivumbi kinatifuka; UDA inaelekea mahakamani kutaka kura za Muguga zihesabiwe upya huku nayo Jubilee ikitaka kura za Kiambaa zihesabiwe tena. Aidha, nani ana ufuasi mkubwa Mlima Kenya baina ya Uhuru Kenyatta na William Ruto? Kuelekea 2022, farasi watakuwa wawili au watatu? Wahariri, Geoffrey Mung'ou na Odeo Sirari wanamshirikisha mwanahabari Victor Mula...

Jul 20, 202127 min

HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Siasa za miungano, kulumbana na kuhamia mirengo

Je, muungano baina ya Jubilee na ODM utaafikia malengo ya kubuni serikali 2022? Aidha, kuhama au kuhamia mirengo ya kisiasa kumeshika kasi nchini bila kusahau joto la kisiasa Mlima Kenya; nani atanufaika au kupoteza kisiasa? Geoffrey Mung'ou, Odeo Sirari na Murimi Mwangi wanayazamia masuala haya.

Jun 24, 202124 min

HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Kura ya maamuzi itafanyika? Maendeleo ni ya kibaguzi? Mung'ou, Zubeida na Odeo wanachanganua

Wakati wa maadhimisho ya Madaraka jijini Kisumu, Rais Kenyatta aliilaumu Idara ya Mahakama kwa maamuzi aliyotaja kuchelewesha utashi wa mwananchi na kuzidisha gharama, mfano kurudia uchaguzi. Je, anakandamiza uhuru wa mahakama? Suala jingine ni iwapo kura ya maamuzi itafanyika au la kwa kuzingatia kesi za kuipinga. Na je, Uhuru anatekeleza maendeleo kwa ubaguzi? Wahariri, Geoffrey Mung'ou, Zubeida Koome na Odeo Sirari wanachambua masuala haya.

Jun 03, 202121 min

Hoja za Wahariri Podcast; Mahakama Kuhusu BBI

Suala la majaji watano wa Mahakama Kuu kuharamisha mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho limechochea gumzo. Aidha, walisema kwamba Rais Kenyatta alikosea katika kuanzisha mchakato wa kuirekebisha katiba badala ya kuanzishwa na wananchi, vilevile kwamba anaweza kushtakiwa. Je, huo ulikuwa uamuzi wa kisheria au kisiasa? Wahariri wetu, Geoffrey Mung'ou, Zubeida Koome na mwanahabari nguli, Duncan Khaemba wamelizamia suala hili kwa kina.

May 15, 202127 min
For the best experience, listen in Metacast app for iOS or Android